January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Constant Omari atiwa korokoroni mwaka mmoja kushiriki michezo

ZURICH, Uswiss

ALIYEKUWA Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka DR Congo (FECOFA), Constant Omari amepigwa marufuku kushiriki shughuli yoyote inayohusiana na mpira wa miguu kwa miezi 1️12 yaani mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Omari alijiuzulu kutoka wadhifa wake huo Jumatano ya Juni 15 mwaka huu, baada ya kuongoza Shirikisho la Soka DR Congo kwa muda wa miaka 18. Kesi rasmi za uchunguzi zilifunguliwa dhidi ya Omari mnamo Januari 7, 2021 baada ya kupokea Euro 66,000, ambayo FIFA imeamuru alipe kama faini.

Mwanachama huyo wa zamani wa Baraza la FIFA alipatikana na hatia ya kupokea pesa hizo wakati wa mazungumzo ya CAF ambayo yeye ndio alikuwa muwakilishi wa Shirikisho dhidi ya kampuni ya Habari ya Ufaransa, Lagardère Group. Adhabu ya Omari inatarajiwa kumalizika Juni 18, 2022.