January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Connie Chiume awapa darasa wasanii Bongo

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MUIGIZAJI mahiri kutoka nchini Afrika Kusini, Connie Chiume ambaye pia ni Muigizaji wa Filamu ya Black Panther, ametoa mafunzo maalum kwa wasanii yaliyoratibiwa na Taasisi ya Refocus Africa kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania.

Mafunzo hayo ya ubobevu (master class) yalilenga kuimarisha uwezo wa Waigizaji kwenye maeneo ya uigizaji, namna ya kutambua kipaji, kuthamini kazi ya Sanaa kwa Muigizaji, ikiwemo nidhamu, pamoja na ushirikiano wa kimataifa katika filamu.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo pamoja na Balozi wa Bodi ya Filamu, Muigizaji Yvonne Cherrie almaarufu Monalisa, waliungana na Wanatasnia ya Filamu katika mafunzo hayo.