Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Coca-Cola imezindua kampeni mpya iitwayo “Chupa la Machupa”, yenye lengo la kuwazawadia mamilioni ya wateja wa vinywaji vya Kampuni hiyo.
Kampeni hiyo, inawalenga zaidi watumiaji wa chupa za glasi zenye ujazo wa mililita 350, inalenga kuwanufaisha wateja na punguzo la bei.
Kupitia kampeni hiyo, wateja watakaonunua vinywaji pendwa vyenye ladha ya Coke, Sprite, Fanta Orange, Fanta Pineapple au Fanta Passion katika chupa ya glasi ya mililita 350, watatakiwa kuangalia chini ya kizibo ili kujua kiwango cha punguzo walichoshinda.

Baadhi ya washindi watapata punguzo la asilimia 100 (yaani soda ya bure), wengine punguzo la asilimia 70 (ambapo watalipa Shilingi 200 tu), na wengine punguzo la asilimia 30 (ambapo watalipa Shilingi 500).
Wateja watalipa tu kiasi kilichoandikwa chini ya kizibo, huku Coca-Cola ikigharamia kiasi kilichosalia kupitia mawakala wake kote nchini.
Pia, Kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi miwili inalenga kuwafikia zaidi ya wateja laki moja (100,000) kila wiki.
Mbali na kuwazawadia wateja, kampeni hiyo pia inalenga kuwawezesha mawakala na wafanyabiashara mbalimbali kuongeza mauzo na kipato chao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Limited, Jonathan Jooste alisema:”Kupitia kampeni ya ‘Chupa la Machupa’, tunawazawadia wateja wetu na kushirikiana na biashara mbalimbali kote nchini.
“Kampeni hii itaendeshwa kupitia maduka zaidi ya 35,000 Tanzania nzima, ikiwa ni uthibitisho wa kasi ya ukuaji wa biashara zetu,” amesema.
Kwa upande wake Meneja Masoko Mwandamizi wa Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo alisema,
“Tunarudisha kumbukumbu za chupa ya glasi ambayo imekuwa kivutio cha matukio ya sherehe nchini Tanzania kwa muda mrefu.
“Coca-Cola daima imekuwa sehemu ya milo ya Jumapili na mikusanyiko ya Krismasi. Kampeni hii ni sehemu ya nyakati hizo muhimu katika maisha yetu ya sasa,” alisema.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo ni zaidi ya kutoa punguzo la bei, bali ni sherehe kwa wateja waaminifu ambao wameifanya Coca-Cola kuwa sehemu ya kila tukio la furaha katika maisha yao.
Iwe ni mchana wa joto kali au kwenye mikusanyiko ya kifamilia, Coca-Cola daima imekuwa ishara ya umoja na furaha isiyo kifani.
Katika kipindi cha kampeni, mawakala wa Coca-Cola watatembelea mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Songea, Njombe, Tanga, Zanzibar, Katavi na Sumbawanga, ambapo watakuwa na fursa ya kuzungumza na wateja pamoja na wafanyabiashara kuhusu kampeni hiyo.
Aidha, wateja watapata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali sambamba na hadithi za kumbukumbu zao za kunywa vinywaji vya Kampuni ya Coca-Cola kama Coke, Fanta au Sprite katika chupa ya glasi.

More Stories
Hospitali ya Amana,kinara utoaji huduma za matibabu
Wenyeviti Ilemela wafunguliwa macho kuhusu wahamiaji haramu
Wadau waitwa kuchangia upauaji Maabara sekondari ya Mtiro