Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online
COCA-COLA Kwanza Ltd, imeadhimisha miaka 30 ya operesheni zake nchini Tanzania, ikiwa hatua muhimu ya safari yenye ubunifu, ukuaji na historia pana ya mchango mkubwa katika ustawi wa nchi.
Historia ya kampuni ya Coca-Cola nchini Tanzania, ilianza mwaka 1952 kufuatia ufunguzi wa kiwanda cha kwanza cha kuzalisha na kupakia vinywaji, kilichojulikana kama Tanganyika Bottlers jijini Dar es Salaam.
Huo ulikuwa msingi wa baadaye wa kampuni ya Coca-Cola Kwanza Ltd.Mnamo 1995, kampuni ya Coca-Cola SABCO (Pty) Ltd ilinunua kampuni mbalimbali za kuzalisha na kupakia vinjwaji, ambapo kwa pamoja vilipewa jina la Coca-Cola Kwanza.
Miaka miwili baadaye, kiwanda cha kilichoko Mikocheni, Dar es Salaam, kilizinduliwa rasmi na Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa mnamo 1997.
Kiwanda hicho kilianzisha utengenezaji wa bidhaa za Coca-Cola za viwango vya juu na mchango wake katika ustawi wa uchumi wa Tanzania ukaanza kuonekana.
Mwaka wa 2016, kampuni ya Coca-Cola SABCO iliungana na kampuni nyinginezo na kuunda kampuni ya Coca-Cola Beverages Africa iliyo na uwepo katika nchini 14.
Coca-Cola Kwanza ni moja ya kampuni zilizo chini ya Coca-Cola Beverages Africa.
“Miongo mitatu ya Coca-Cola nchini Tanzania ni safari ya mafanikio na tumejitolea kuendelea na ukuaji thabiti na mchango chanya kwa jamii.
“Tutaendelea kuwekeza kwa watu, shughuli zetu na jamii ya Watanzania ambao tunahudumia,” amesema David Chait, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza.
Katika kipindi cha miongo mitatu, kampuni ya Coca-Cola Kwanza imepanua shughuli zake na ina viwanda jijini Dar es Salaam na Mbeya.
Kampuni ya Coca-Cola Kwanza ilitambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika utoaji wa ajira kwa idadi kubwa ya Watanzania, na sera mwafaka zinazolenga maslahi ya wafanyakazi.
Kupitia maadhimisho hayo
kampuni inasherekea mafanikio kwa pamoja na wafanyakazi wake, wadau, wawakilishi wa serikali, wateja na jamii ya Watanzania.
“Tunapoangalia mbele, kampuni ya Coca-Cola Kwanza itazidi kuchangia katika uchumi jumuishi, kuboresha ushirikiano nchini, kuwekeza katika uzalishaji endelevu na kuendelea kuhudumia mamilioni ya Watanzania kwa vijwaji vya ubora wa juu kote nchini ,” ameogezea Chait.
Kampuni ya Coca-Cola Kwanza kwa sasa imeajiri watu 500. Mamia maelfu ya wengine, kama vile mawakala, wasambazaji, wauzaji wa bidhaa za Coca-Cola pia wamenufaika na ajira na kujistawisha kiuchumi.
Ukuaji huo unadhihirisha mchango mkubwa wa kampuni ya Coca-Cola Kwanza katika uzalishaji wa ajira na ustawishaji wa uhumi wa Tanzania.
Kando na biashara zake za msingi, Coca-Cola Kwanza imehusika pakubwa katika miradi ya kuinua jamii katika sekta za elimu, uwezeshaji wa vijana na uboreshaji wa maziingira.
Miradi hiyo inadhihirisha wazi juhudi za kampuni ya Coca-Cola Kwanza katika kuchangia maendeleo ya Tanzania kiuchumi na kijamii.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina