Na Jackline Martin, TimesMajira Online
CHUO kikuu Huria (Open University) kimeendelea kupiga hatua kwa kuimarisha zaidi mifumo yake ya utendaji na kufundisha huku msisitizo mkubwa ukiwa katika matumizi ya TEHAMA.
Hayo yalisemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa chuo hicho Elifas Bisanda wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 30 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake Desemba 1992 ambapo kilele chake kinatarajiwa kuwa mwezi Novemba 28 mwaka huu kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma
Bisanda alisema chuo hiko kimefanikiwa kuongeza idadi ya wahitimu kutoka 22,289 mwaka 2014 hadi wahitimu 49,830 mwaka 2021 ambapo Katika idadi hiyo jumla ya wahitimu 7,335 ni wa ngazi ya Shahada za Uzamili, Uzamivu na za Heshima.
Pia alisema Katika kipindi cha miaka 30 ndani ya chuo hicho jumla ya wahitimu 49,830 wametunikiwa vyeti vya shahada mbalimbali huku udahili wa wanafunzi kwa mwaka umeongezeka kutoka asilimia 8.3 mwaka 1994 hadi asilimia 38.1 mwaka 2019/2020.
Aidha alisema Wakati wa janga la UVIKO-19, CKHT kilikuwa Chuo Kikuu pekee nchini ambacho kiliendelea na shughuli zake kama kawaida bila kuathiriwa na hilo janga.
Bisanda alisema CKHT kupitia kitengo maalum cha Teknolojia Saidizi (Assistive Special Technology Unit – ASTU), kimeendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika maeneo mbalimbali nchini.
“Mafunzo haya yamejikita katika kutoa ujuzi wa kutumia vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa watu wasioona, viziwi, wenye uoni hafifu, na walemavu wa viungo.”
“Baada ya mafunzo, wanafunzi hawa wameweza kutumia
kompyuta, simu janja, vishkwambi, na mifumo mbalimbali ya TEHAMA kama vile mfumo wa kujifunzia wa Moodle Learning Management System. Zaidi, viziwi wamepata utaalamu wa kutengeneza mifumo ya mawasiliano ya kompyuta. Wenye
ualbino ambao wana ulemavu zaidi ya mmoja (kama vile haoni vizuri wala kusikia vizuri) wameweza kutengeneza Tovuti kwa ajili ya taasisi mbalimbali.”
Alisema Kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu 2024 takriban wanafunzi 270 wameshapata mafunzo
hayo
“Kwa mfano, yupo mhasibu asiyeona aliyejifunza kutumia mifumo ya TEHAMA pamoja na mifumo ya serikali kama vile e-Office Management System na Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE). Pia Daktari Profesa asiyeona kutoka Chuo cha Muhimbili
amepata mafunzo ya kutumia mifumo ya TEHAMA kutoka katika kitengo chetu maalum cha Teknolojia Saidizi hapa CKHT”
Mbali na hayo, Bisanda alisema walifanikiwa Kukamilika kwa tovuti ya Lugha ya Alama ya TEHAMA kwa wanafunzi wasioona ili
kuwasadia kujiendeleza kwa kutumia TEHEMA.
Pia alisema walifanikiwa kufanya maandalizi ya kutengeneza vitabu vinaongea (Talking books) kwa ajili ya
watu wasioona.
Kadhalika, Bisanda alisema kupita Mradi wa HEET, CKHT kilipewa kiasi cha Shilingi 20.7 bilioni kwa
ajili ya miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa maabara saba za sayansi za kisasa mikoani, kusomesha wanataaluma nk.
Pia Bisanda alisema walifanikiwa kukamilisha Mradi wa ujenzi wa majengo mapya na miundombinu kwenye Vituo vya Mikoa vitano ikiwemo Geita, Lindi, Kigoma, Manyara na Simiyu) ambapo mradi huo ulighagharimu kiasi cha
Shilingi 1,802,745,287.50 ambazo zilitolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Teknolojia.
Kuhusu kilele hiko, ambacho kimeenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘ Miaka 30 ya kufungua fursa endelevu za elimu kwa njia ya masafa na Huria’ Bisanda alizitaja baadhi ya shughuli ambazo zitafanyika ikiwa ni pamoja na kuandaa mihadhara ya umma na makongamano ga mawazoni ambapo mada mbalimbali zinawasilishwa na kujadiliwa lakini pia kufanya maonesho ya kitaalhma yatakayoandaliwa na kuratibiwa na vituo kurugenzi na vituo vya mkoa n.k
Miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho walisema wanajuvunia kusoma chuo hicho kwani unawapa uwanja mpana wa kufanya kazi na kusoma kwa wakati
“chuo hiki kinanisaidia kulingana na muda wangu kinanisaidia kufanya majukumu yangu mengine kwa sababu hainibani kwenye ratiba muda wowote ninaweza kusoma kwa sababu ni Online”alisema Salha
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja