Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online, Dar
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), cha jijini Dar es Salaam, kimepongezwa kwa ubunifu mkubwa kwenye njanja mbalimbali za kitaaluma hasa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (Tantrade), Latifa Mohamed, alipokuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la 57 la kitaaluma chuoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda kwenye maonesho chuoni hapo, Latifa alisema chuo hicho kimepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali za kiteknolojia.
“Mimi nimesoma hapa kozi ya masoko hivyo nina ushuhuda wa maendeleo makubwa yaliyofikiwa chuoni hapa. CBE nimeona umuhimu wa kutumia teknolojia natoa wito kwa watanzania wote wawalete hapa kwasabbu hawa wana kozi zinazokwenda na wakati kwenye soko,”amesema
Amesema kwenye maonesho ameona ubinfu mbalimbal na alitoa wito kwa taasisi zianzazodhamini wabinifu kufika choni hapop kuangalia vijana wa chuo hicho walivyo mahiri.
Amesema ameshangazwa na ubunifu wa vijana wanaosoma Teknolojia ya Habari na Mawasiliano chuo ni hapo Tehama kwa namna walivyobuni mfumo unaomwezesha mtu kuzima taa au kifaa chochote cha umeme kwa kutumia simu
“Mfano unaweza kusahau kuzima mashine ya kufulia au kifaa chochote kinachotumia umeme lakini kupitia ubunifu huu wa vijana hawa unaweza kuzima kwa kutumia simu yako ya mkononi ukiwa popote pale, haya si maendeleo madogo ni mambo makubwa sana,” alisema.
Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema, aliwataka wanajumuiya ya chuo hicho kutembea kifua mbele kwani chuo hicho kimekuwa kikifanya mambo makubwa kitaaluma.
Pofesa Mjema amesema kuna umuhimu wa kuyatangaza mambo mazuri yanayofanywa na chuo hicho kwani yako mengi ila bado hayajafahamika ipasavyo kwa jamii.
“Tuko vizuri sana na nawaomba mjidai kwasababu kuna watu hata wanaulizia flana za CBE zinapatikana wapi wakanunue sasa ukishaona watu wanataka kujinasbisha nawewe ujue mambo yako ni mazuri sana,” alisema
“Kwasababu kwa kawaida mtu ukiwa na hela au maisha mazuri kila mtu atasema Yule ni ndugu yangu lakini ukiwa lofa au mwizi hakuna atakayependa kujinasbisha nawewe kwanza hatataka watu wajue kwamba mna undugu, lakini sisi watu wengi kwa sasa wanapenda waonekane wako nasisi” amesema
Amesema chuo hicho kitaendelea kufanya makubwa kuanzia kwenye tafiti mbalimbali ili kujitofautishe na wengine ambao wamekuwa wakifanya mambo yakawaida kwenye jamii.
Profesa Mjema amesema CBE imekuwa ikifanya vizuri kwa kuandaa na kufanya tafiti mbalimbali na kutoa machapisho ya kitaaluma ambayo yamekuwa na msaada kwenye ufundishaji.
Amesema wahitimu wa chuo hicho wamekuwa na uwezo wa kufanya mambo makubwa maeneo yote wanayokwenda kufanya kazi hali ambayo inakipandisha chuo hicho kwenye hadhi ya vyuo vikuu duniani.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa