January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano

Na Esther Macha,Timesmajira Online,Chunya

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi,Maryprisca Mahundi(Mb) ametembelea Kituo cha mkongo wa Taifa cha mamlaka ya mji mdogo wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kilichojengwa kwa lengo la kuboresha mawasiliano na ili kuongeza ufanisi kwa watendaji wa serikali katika makusanyo ya Serikali.

Mhandisi Mahundi amesema  hayo alipotembelea kituo cha Mkongo wa Taifa cha Mamlaka ya Maji Mdogo Makongolosi wilayani Chunya ambacho kimejengwa kwa lengo la kuboresha mawasiliano

Aidha Mhandisi Mahundi amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya mawasiliano kupitia ujenzi wa vituo vya Mkongo wa Taifa.

“Nampongeza Sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kwa jitihada hizi anaendelea kuzifanya katika kuboresha mawasiliano nchini  kwenye Mkongo wa Taifa vya nchi kavu na baharini, na kupitia uwekezaji huo wilaya 139 nchini zitanufaika na huduma ya Mkongo wa Taifa hivyo kurahisisha utendaji wa serikali “amesema Mhandisi Mahundi.

Kwa upande wake Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya na Songwe ,Mhandisi Mujuni Kyaruzi amesema mkongo huo utaunganisha mkoa wa  Mbeya na mkoa wa Songwe kupitia Wilaya ya Songwe ambapo unatarajiwa kuanza kutumika mwezi Aprili mwaka huu baada ya kukamilika ufungaji wa waya eneo la kilomota 10 lililobaki.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Alhaj Batenga amesema wananchi wachangamkie fursa hiyo ya ujiio wa mkongo wa Taifa kwani kwa sasa kumekuwa na changamoto ya ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali kutokana  na changamoto ya mawasiliano maeneo mengi ya Wilaya hiyo, huku akiwataka wananchi kuilinda miundombinu hiyo ili Taifa liendelee kukua kiuchumi.