Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo amewataka Wakuu wa shule zote zinazomilikiwa na Umoja wa Jumuiya ya wazazi ya chama hicho kuendelea kujenga nidhamu katika shule wanazoziongoza ili kuendelea kujenga heshima ya CCM.
Amesema kuwa heshima ya mwalimu ni matokeo bora hivyo amesisitiza kuongeza juhudi katika kuleta ufaulu zaidi na kuhaidi kuwa awamu ijayo watatoa zawadi kulingana na kiwango cha ufaulu katika shule husika.
Chongolo amesema hayo jijini hapa leo Julai 15,2022 wakati akiongea kwenye kikao cha Wakuu wa shule za Umoja wa Jumuiya ya wazazi Tanzania ambapo amese ma Jumuiya hiyo imeadhimia kuboresha shule zote zinazomilikiwa na Jumuiya hiyo kuwa zenye viwango,vigezo, vipimo na utofauti ili kuingia kwenye ubora wa ushindani sawa na shule nyingine na kutaka maboresho hayo kuhusisha makundi kundi yote ikiwemo wanafunzi wenye ufaulu mzuri,ufaulu wa kati na wale wasiojiweza kabisa .
Amesema lengo la chama kuanzisha shule zake ni kuwezesha vijana wote kupata elimu iliyobora ambapo katika matokeo ya mtihani mwaka huu karibu asilimia 80 hadi 90 ya wanafunzi wanaosoma katika shule zinazomilikiwa na chama wamepata ufaulu wa daraja la kwanza na la pili huku mwanafunzi mmoja tu akipata ufaulu wa daraja la nne.
Pamoja na kuongeza wigo wa elimu kwa wananchi waliokosa fursa kwenye machaguo mbalimbali ya serikali,kupanua wigo na kupata wasomi wengi kwenye nchi na kuongeza kiwango chenye elimu yenye tija nchini.
“Kazi bado haijaisha,tuna kazi nyingine ya ziada,bado lengo kuu la elimu bora na kufanikisha kuendelea liko pale pale
kufanikisha misingi ya uanzishaji wa shue zetu kwa kuwaandaa na kuwajengea msingi wanafunzi walioshindwa na wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki,
“Ili kuendana na malengo ya kuanzisha shule hizo inatakiwa kila kundi lipewe dozi kulingana na hali halisi ya madaraja yenu na kwasababu kila jambo linahitaji msukumo zaidi wa mafanikio,
“Sasa hivi hatupo tena kwenye giza,
tunatakiwa kuongeza bidii kwenye haya mafanikio tuliyoyaleta wenyewe
na lazima mfahamu kuwa hakuna muujiza kwenye mafanikio,”amesema.
Katibu Mkuu huyo pia amesema kulingana na mwenendo wanaoenda nao shule hizo zinahitaji mabweni hivyo kuweka wazi kuwa yeye kwa nafasi yake atahakikisha anatekeleza jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya walimu na wale wanafunzi wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki.
“Ahadi yangu ipo palepele kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri zaidi ili kuendana na hadhi ya Jumuiya hii ikiwa ni apamoja na kuongeza madarasa mawili mawili,tutaangalia pia uhitaji wa shule husika hali itakayoongeza ufanisi na kupekelea shule zetu kuwa kimbilio kwa kila mtu,”amesisitiza Chongolo
“Tumewapa jukumu hili la kuboresha mazingira ya elimu,nendeni mkalifanye kwa dhamira ya dhati,mengi mmefanya kwa kujitolea,mafanikio yanatafutwa na ili kufanikiwa lazima uweke juhudi zako ninyi ni watu wa msukuko tambueni heshima ya Mwalimu ni matokea,ukitaka kuheshimiwa tengeneza matokeo yako vizuri,”amesema na kuongeza;
Heshima ni gharama,na ninyi mmeonesha namna mnavyodhamiria kuitafuta heshima kwa gharama yoyote,sina shaka dhamira yenu ni kujaza kibaba”amesisitiza
Katibu huyo pia alitoa wito kwa Wakuu wa Shule hizo za Jumuiya ya wazazi kuwapa motisha walimu na wanafunzi ili kufanya vizuri zaidi na kwamba awamu ijayo hawatatoa zawadi kwa usawa bali watatoa kutokana na ushindi wa matokeo
“Tutatumia ushindani wa vigezo,vipimo, viwango na utofauti,tusilazimishe mambo makubwa tuendelee kuweka msukumo na viwango vyetu ili tupate ubora tunautaka,”amesisitiza
Pamoja na hayo Katibu huyo Mkuu wa CCM ametumia nafasi hiyo kuwataka Wakuu hao kupenda kufanya kazi kwenye mazingira yanayohitaji mafanikio na kukemea tabia ya baadhi ya walimu kutamani shule zilizofanikiwa.
“Mwalimu mwenye uwezo apelekwe kwenye shule inayohitaji mafanikio,hali hiyo itawaheshimisha walimu,kila mtu atafute mafanikio ya shule yake nisione mtu anataka kuhamia shule yenye mafanikio waliyoyaanzisha wenzie wakati yeye ameshindwa huo ni ubinafsi mkubwa,”amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa Dkt.Edmund Mndolwa amesema nafasi hiyo kuwataka Wakuu wa Shule hizo kuacha kuingiza siasa kwenye Jumuiya hiyo huku akiwataka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadali na uzalendo.
“Siasa ina mahali pake hatupaswi kuiingiza kwenye utendaji,lazima tujue kutofautisha vitu hivi,najua kuna wakati mnafanyia kazi katika mazingira magumu lakini msikate tamaa ili muendelee kuijenga heshima yenu,”amesema
Amesema shule za wazazi nchini kwa sasa zina utulivu wa kutosha tofauti na ilivyokuwa mwanzo na kueleza kuwa hali hiyo imetokana na maelekezo ya uongozi uliopo na kufanya matokeo mazuri
kwa shule zote za wazazi licha ya wanafunzi waliopo ni wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja