December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CHONGOLO apongeza hatua ya Jengo la Tanzanite City Mirerani

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mirerani

KATIBU Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amekagua ujenzi wa mradi wa jengo la soko la madini Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara (Tanzanite City) na kupongeza hatua iliyofikiwa ya mradi huo.

Hayo alibainisha jana wakati akikagua jengo hilo amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha za kujenga jengo hilo.

Chongolo alisema amekagua ameona uhalisia wa jengo hilo kuwa limefikiahatua nzuri likikamilika wafanya wataingia kufanya kazi zao na hatimaye kuwezesha Mji Mdogo wa Mirerani kuchangamka zaidi kiuchumi.

“Jengo limefikia hatua nzuri, lilikamilika wafanyabiashara wataingia kufanya kazi na kupelekea Mji Mdogo wa Mirerani kuchangamka zaidi kiuchumi,” amesema Katibu Mkuu Chongolo.

Meneja wa shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Kilimanjaro, Juma Kiaramba akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Chongolo amesema ujenzi wa jengo la soko la madini Mirerani umefika hatua ya asilimia 53 ya ukamilishaji wake ambapo utagharimu jumla ya shilingi 5,494,724,533.28.

Kiaramba amesema mkataba huo ni wa miezi 15 kuanzia Machi 2022, usanifu umeanza Machi 22 na ujenzi ukaanza Mei 22 mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika Mei 21 mwaka 2023.

” Usanifu uliofanywa ni wa ghorofa tano ila ujenzi kwa awamu ya kwanza ni ghorofa tatu, hata hivyo mazungumzo yamefanyika kati ya mkandarasi na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ambapo shirika litajenga ghorofa ya chini na ghorofa nne na kufanya umaliziaji wote wa sakafu ya chini kufanya baadhi ya kazi kubwa katika sakafu ya kwanza kwa gharama ile ile ya awali” amesema Kiaramba.

Aidha alisema kazi zilizokamilika ni pamoja na maandalizi yote muhimu ya awali yanayohitajika kabla ya ujenzi kuanza, ujenzi wa sakafu mbili za awali na upigaji wa plasta kwa sakafu ya kwanza kwa ndani nao umekamilika.

Akizutaka kazi zinazoendelea ni pamoja na ukamilishaji wa ujenzi wa sakafu ya tatu, manunuzi na kuhakiki vifaa vyote muhimu vya ujenzi vinavyohitajika, ujenzi wa ukuta wa tofali wa sakafu ya kwanza na ujenzi wa ukuta wa nje kuzunguka jengo.

Akizungumzia changamoto zianazowakabili alisema ni kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi kila mara ni moja ya changamoto za kuongezeka kwa gharama za ujenzi kwa upande wa shirika.

Amesema katika kujikwamua na changamoto hiyo shirika limekuwa likifanya manunuzi pamoja moja kwa moja kwenye maeneo ya uzalishaji.

“Ni matarajio ya shirika kuwa litakamilisha mradi huu muhimu kwa wakati na kwa kiwango tarajiwa kwa ushirikiano na mshitiri, ofisi ya DED Simanjiro na Mkoa wa Manyara kwa ujumla,” amesema Kiaramba.

Hata hivyo amesema hali hiyo imelenga kuzuia ucheleweshaji kazi unaoweza kusababisha ongezeko zaidi ya gharama za ujenzi.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba akitoa taarifa ya Utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Soko la Madini Mirerani ( Mirerani Tanzanite City ) Kwa Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo alipolitembelea nankukagua soko hilo wakati wa mwendelezo wa ziara yake kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Picha na Mary Margwe
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba akitoa taarifa ya Utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Jengo la Soko la Madini Mirerani ( Mirerani Tanzanite City ) Kwa Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo alipolitembelea nankukagua soko hilo wakati wa mwendelezo wa ziara yake kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Picha na Mary Margwe