December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chongolo akemea wanaosaka ubunge sasa

Na Mwandishi wetu,timesmajira, Online

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wanachama kuanza kujipitisha katika majimbo kutafuta wapambe ili wawasaidia kwenye malengo yao ya Ubunge na udiwani kwa mwaka 2025.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Chama hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa taratibu, kanuni na katiba ya CCM ili kuwadhibiti watu hao, kwani muda wa uchaguzi bado na sasa kila jimbo lina mbunge na kila kata kuna diwani hivyo ni vema kwa kila mwanachama kusubiri muda ufike na sio kuanza sasa wakati viongozi waliochaguliwa wanafanya kazi ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.

Katibu Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo tarehe 13 Julai, 2022 wakati akifungua kongamano la Mafunzo ya Uongozi kwa mabalozi wa mashina na viongozi wa matawi mkoa wa Dodoma .