Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
MKuu wa Mkoa Dar-es-Salaam Albert Chalamila, ametoa wiki moja kwa watu waliopora au kutapeli ardhi na mali za wananchi mkoani humo kuzirejesha huku akisisitiza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya watakaokaidi agizo hilo.
Chalamila,ametoa agizo hilo,Machi 2,2026 mkoani Dar-es -Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari,ambapo amesema wamebaini kwamba kuna kiwango kikubwa cha kutapeli na unyang’anyi wa ardhi kwa wananchi.
Ambapo amedai kuwa yapo makundi makubwa ambayo yanafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya watu wengi nje na hata ndani ya mifumo ya kiutendaji.
Hivyo amesema,wamefanya uchunguzi wa kina ambapo wanayo orodha ambayo wameithibitisha ya baadhi ya watu ambao ndio wamekuwa wanyang’anyi wakubwa wa ardhi katika Mkoa wa Dar-es-Salaam.
“Nawapatia wiki moja ili wahakikishe zile ardhi ambazo wamezikalia ambazo siyo za kwao wazirudishe kwani tumeisha fanya uchunguzi wa kina.Mpaka sasa tu ardhi si chini ya 19,ambazo zimerudishwa kinyemela nyemela,na wale wote waliopora ardhi hizo,tumeshaurina na kuwasamehee kwa kuwa wamerudisha ardhi hizo kwa wahusika,”amesema Chalamila.
Amesema kutokana na jambo hilo,watu wengi na makundi mengi wanalia ikiwemo kundi la wajane,warithi ambao wamefiwa na watoto zao au wazazi,ambapo makundi hayo yamekuwa yakinyang’anywa ardhi na mali zingine.
Pia wamegundua utapeli mwingine katika sehemu(showroom) za kuuzia magari,ambapo watu wanalipia magari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania lakini wengi wanadhulumiwa magari yao wakidai kuwa bado yapo bandarini.
“Lakini ukifuatilia magari hayo hayapo bandarini na ukitakuta yanakuwa bado hayajalipiwa chochote,”amesema Chalamila.
Hata hivyo amesema anayo mifano michache ikiwemo ya mtu mmoja kudhulumiwa kiasi cha shilingi milioni 100,huku eneo jingine la unyang’anyi ni la mikopo umiza.
“Ipo baadhi ya mikopo watu wanakopeshana,anakopa leo,anasaini mkataba wa mkopo leo,lakini muda huo na leo hiyo hiyo anasaini mkataba wa kuuza eneo lake,”amesema Chalamila na kuongeza:
“Maana yake kwamba anawekewa masharti kuwa ifikapo kesho saa tisa ardhi hiyo,nyumba hiyo au kitu alichoweka dhamana kitauzwa,wanasaini mikataba yote miwili,hapo pia tumegundua kuwa Kuna unyang’anyi,watu wanaachia mali zao kwa sababu ya mikopo umiza,”.

More Stories
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria