Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbeya
CHAMA cha kutetea Haki na maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA) kimesema kuwa kimesikitishwa na sehemu ya hotuba ya TUCTA kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambayo ilikuwa na kipande chonganishi ikimuomba Rais arekebeshe sheria ili wafanyakazi wakose uhuru wa kuanzisha vyama vingine.
Kauli hiyo imetolewa Mei 5,2025 na Katibu Mkuu wa Chama cha kutetea Haki na maslahi ya Walimu Tanzania(CHAKAMWATA)Meshack Kapange wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya Chama hicho yaliyopo eneo la Mafiati Jijini Mbeya kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa ilifanyika Mkoani Singinda.
Kapange amesema kuwa kitendo kilichotaka kutokea ni uchochezi wa wawazi na hauwezi kuvumiliwa hivyo wanaaamini risala hiyo kabla ya kusomwa ilipita kwenye vyombo vya ulinzi na usalama na kukaguliwa kabla ya kwenda kusomwa kwa Rais na mawaziri pia walikunayo kabla haijaruhusiwa kusomwa kwa Rais.
“Kumwambia Rais aruhusu kubadilisha sheria uhuru wa vyama vya wafanyakazi hauanzii kwenye sheria bali unaanzia kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mh Rais ni binadamu angekosa tu hekima na kujibu hebu shughulikieni hilo tayari ilikuwa ni taflani kwenye nchi hii tungelaumu Rais kuwa Rais amevunja katiba lakini angekuwa amesabishwa na watu hawa ,tumeona tusikae kimnya tutoke hadharini kuwaambia TUCTA na wanachama wake kuwa kitendo cha kutaka kumpotosha Mh Rais kumtaka kutoa maelekezo ya kuvunja katiba ya nchi ambayo ameapa kuilinda “amesema Katibu Mkuu huyo.
Akizungumzia kuhusu Rais Dkt .Samia kupandisha kiwango cha mshahara kwa watumishi,Kapange amesema kuwa wanamshukuru kwa ongozeko hilo la mshahara.
Hata hivyo amesema kwamba . kupandisha kwa kiwango chamshahara ni historia kwa Tanzania kwani haijawahi kutokea kwani Rais Samia amegusa maisha ya watanzania walio wengi.
“Sisi wafanyakazi ni mikono ya watanzania wengine ya kuchumia fedha hatuli fedha kama fedha tunakula mahindi,matembele,bamia ndo vyakula vyetu,tukilipwa vibaya tunakwenda kwa watanzania wenzetu maskini kwenda kununua vitu vibaya,tukilipwa vizuri tunakwenda kununua vizur unamkuta Bibi hajui nguo alifua lini bado unabembeleza bado akupunguzie lakini ukilipwa vizuri utanitumia yule bibi utaangalia maisha yake yalivyo ,hivyo kubadilisha mshahara kwa wafanyakazi kunabadilisha maisha kwa jamii na Taifa kwa ujumla “amesema Kapange.
Mmoja wa Walimu ambaye hakutaka jina lake kuandikwa amesema kuwa kitendo cha kuongezeka kwa mshahara kimewapa faraja sana watumishi wa umma .
“Rais Samia amejua kutukosha kwa ongozeko la mshahara kiukweli hasa sisi walimu tumepata faraja kubwa kwani haijawahi kutokea hivyo ongozeko hili limetupa ari ya kufanya kazi zaidi kwa kujituma “amesema .
More Stories
Magugu maji yatajwa changamoto ya uzalishaji umeme maporomoko Rusumo
Wataalam Maendeleo ya Jamii waaswa kutoruhusu tamaduni potofu
CCM yatoa salam za pole kifo cha Msuya