Na Mwandishi Wetu
MWENYEKIT wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,amewasihi Waislamu waendeleze mema yote waliyokuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu na kuyaishi wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwemo haki, upendo, neema na rehema katika jamii nzima.
Mbowe ametoa kauli wito huo Jumamosi wakati wa Kikao cha Kamati Kuu ambacho kimefanyika kwa njia mtandao.
“Tunawasihi Watanzania wote kusheherekea kwa amani na utulivu. Tunaendelea kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia tahadhari zote za kujikinga dhidi ya Ugonjwa wa COVID-19.”
Tunaomba kila Mtanzania atambue kuwa hatua ya kwanza kabisa ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona ni kuanza na mtu binafsi. Kilo mmoja wetu ndiye mwenye wajibu kwanza wa kujilinda na kuwalinda wengine, dhidi ya maambukizi ya Corona,” amesema Mbowe.
Katika kikao hicho Kamati Kuu ilijadili masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 katika mazingira ya uwepo wa Janga la Corona, nchini.
Taarifa hiyo ilieleza kwamba CHADEMA imeendelea kufanya shughuli zake za kisiasa, huku ikizingatia tahadhari ya kupunguza mikusanyiko ikiwa ni njia mojawapo inayoshauriwa na wataalam wa afya kujikinga dhidi ya Corona.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam