Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dsm
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kinatarajia kuzindua Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa mkutano unaotarajia kufanyika katika Uwanja wa Zakhiem Mbagala, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, kesho chama hicho kitafanya mkutano wake mwingine kwenye Uwanja wa Tanganyika Parkers, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Agosti 30, 2020, chama hicho kitafanya mkutano wa tatu jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Tabata shule ya msingi Segerea, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni na baadaye kitahamia mikoani.
Mikutano mingine ya chama hicho itafanyika kama ufuatavyo; Agosti 31, 2020, Uwanja wa Relini, jijini Arusha, kuanzia saa 400 asubuhi hadi saa 12.00, Sepetemba 1, 2020, Uwanja wa Furahisha, Kitangili, jijini Mwanza, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni na Septemba 2, 2020, Uwanja wa Lubaga Joshoni, Manispaa ya Shinyanga, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
Septemba 3, 2020, chama hicho kitafanya kampeni zake Uwanja wa Chipukizi, Tabora mjini, kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni, Septemba 4, 2020, Uwanja wa Uhuru, jijini Dodoma, Septemba 5, 2020, Uwanja wa Rwandanzovwe, jijini Mbeya na Septemba 6, 2020, Uwanja wa Sabasaba, mjini Mtwara.
Mikutano ya chama hicho, itaendelea Septemba 7, 2020, Uwanja wa Gombani, Chakechake, Pemba, kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana. Uwanja wa Maisara, Unguja, kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 12.00 jioni.
Tunatanguliza shukrani zetu, tukikuahidi ushirikiano na kutarajia hivyo kutoka kwako na chombo chako kwa ujumla katika kuimarisha demokrasia nchini kwetu ikiwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Watanzania wote.
More Stories
TARURA Kilimanjaro yatimiza ahadi ya Rais Samia
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime