November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chadema: hali ya siasa haijatengemaa

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

DIWANI Mstaafu wa kata ya Tabata na Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la segerea Dar es salaam Patrick Asenga amesema hali ya kisiasa nchini bado haijatengemaa kutokana na kutokuwepo kwa mabadiliko ya mifumo ya kiutawala ya kisheria.

Akizungumza hayo jijini wakati wa mahojiano na TimesMajira TV na Gazeti la Majira amesema kisiasa nchini hali haijawa vizuri kufuatia watu kuendelea kubambikiwa kesi, kutekwa na kucheleweshwa madai ya katiba mpya.

“Hali ya kisiasa nchini bado haijatengemaa kufuatia kufanyika usanii wa kisiasa, kutekwa,mabadiliko ya mifumo ya kiutawala ya kisheria ambavyo inaonekana kushika hatamu ndani ya CCM kila kukicha.

Aidha Asenga ameeleza kumekuwepo ubadhilifu mkubwa maeneo mbalimbali ikiwemo bandari kuwamilikisha wageni,mradi wa magari yaendayo kasi na katika bwawa la ufuaji wa umeme la mwalimu Nyerere.

Mkuu huyo amedai mifumo iliyowekwa na chama cha mapinduzi CCM ya kisheria ni kandamizi kiasi kwamba kinawalinda na kuwanufaisha wachache ndani ya chama hicho.

Hata hivyo kupitia chama chake cha demokrasia na maendeleo Chadema kikimpa ridhaa atagombea ubunge katika kata ya Segerea mwaka 2025.

Kutoshiriki uchaguzi ameeleza ukimsusia nyani shamba la mahindi atapata nafasi ya kula yote hivyo kama mwanachama wa CHADEMA hawataweza kususia uchaguzi ila tutakuja na mbinu nyingine za kukabiliana nao.

DIWANI mstaafu wa kata ya Tabata na Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la segerea Dar es salaam Patrick Asenga akieleza hali ya siasa nchini