Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kusitisha ziara, mikutano, semina na makongamano yanayowahusisha wajumbe wa vikao vinavyopigia kura za maoni wagombea kwa ngazi zote hadi baada ya kura za maoni.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu w CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi imeeleza kuwa, chaa hicho bado kinaendelea na maandalizi ya mchakato wa ndani wa uteuzi wa ndani wa wanachama watakaojitokeza kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwenye Uchaguzi Mkuu 2025 kupitia CCM.
Pia imeeleza kuwa, mchakato wa ndani ya CCM utausisha zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu, vikao vya awamu ya kwanza vya uchujaji na uteuzi kwa ajili ya upigaji wa kura za maoni na kisha vikao vya uchujaji na uteuzi wa mwisho wa wagombea wa CCM kwa nafasi husika.
CCM inaendelea kusisitiza kuwa, mwanachama yeyote anayetarajia kugombea au wakala wake, kuepuka kufanya vitendo vyovyote vinavyoonekana wazi kuwa ni kinyume cha katiba, kanuni na miongozi ya chama hicho.
Aidha CCM inawatakia, viongozi, Watendaji na Wanachama wake kuendelea kusimamia maadili na nidhamu ya chama hicho wakati wote wa maandalizi ya mchakato wa ndani na utekelezaji wa shughuli za uteuzi wa wagombea wa CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2025, huku chama hicho kikisisitiza juu ya umoja, amani na mshikamano ndani ya chama hicho.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi