Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online
CHAMA cha Mapinduzi CCM ,kimepokea kwa masikitiko kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Kilimanjaro Vicky Swai kilichotokea Mei 31 ,2021 moshi mkoani Kilimanjaro.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho,Shaka Hamdu Shaka ilisema Mwenyekiti wa Chama hicho ambaye ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemtaja marehemu Vicky Nsilo Swai kama mwanasiasa mahiri ,mpambanaji mwenye msimamo thabiti wakati wa uhai wake.
Alisema pia Vicky alikuwa mstari wa kupigania usawa wa kijinsia ,utu na adhi ya mwanamke.”Marehemu mama Vicky alitumia sehemu kubwa ya uhai wake kuwaunganisha wanawake wa Tanzania na kuwahimiza katika kushiriki shughuli za maendeleo kisiasa ,kijamii na kiuchumi,”Ilisema sehemu ya taarifa hiyo
Aidha taarifa hiyo ilisema Mama Vicky amewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Kilimanjaro,pia akiwa mke wa Muasisi wa Chama hicho marehemu Asanterabi Zephaniah Swai alishiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika pamoja na kusiadia ukombozi wa mataifa mengine kusini mwa Bara la Afrika.
“Miongoni mwa sifa kubwa alizowahi kuwa nazo Marehemu Vicky Swai,ni uaminifu ambapo amewahi kuhifadhi viatu vya mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Afrika Kusini Hayati Mzee Nelson Mandela kwa miaka 33 kuanzia mwaka 1962 vilipoachwa na mpiganaji huyo wa ANC kwa familia ya Mzee Swain a kuvikabidhi kwake mwaka 1995 akiwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini,”alisema Samia Suluhu Hassan katika taarifa yake.
MWISHOOO
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa