December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yalaani Mbunge Catherine kuvamia maziko ya mfanyabiashara Arusha

Na Mwandishi wetu,Timesmajira,Online

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimechukizwa na kulaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige.

CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Halmshauri Kuu ya Taifa Itikadi,Shaka Hamdu Shaka amesema
Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM.