December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM watakiwa kuvunja makundi

Na Zuhura Zukheir, TimesMajira Online, Iringa

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Abel Nyamahanga, amewataka wanachama wa chama hicho, kuondoa makundi ili waunganishe nguvu za kutafuta ushindi na kumpa kura nyingi mgombea wa CCM, Rais Magufuli, Mbunge Cosato Chumi na madiwani wate wate.

Nyamahanga amesema, Chama Cha Mapinduzi kimefanya upembuzi wa ubunge na kuona kama Cosato Chumi anatosha kugombea kwa msimu huu na sio wengine hawafai bali katika nafasi waliokuwa wanahita ilikuwa ni moja.

Hata hivyo, Nyamahanga anasema uongozi sio sehemu ya kwenda kutajirika bali ni utumishi ambao Chumi kwa muonekano wake anasifa hizo kwa kuwa ni muadilifu, mnyenyekevu na mtu mwenye hofu ya Mungu.

Anasema, Chumi ana madiwani wa CCM, ambao wanania ya dhati ya kwenda kuunganisha nguvu, serikali na wananchi ili kuondoa umasikini, ujinga na maradhi na ndio maana mgombea huyo amesimama kifua mbele kuiomba serikali kuruhusu usafilishaji wa mazao ya misitu ufanyike masaa 24 ombi ambalo lilikubaliwa na rais, hivyo hakuna sababu ya kuto kuwapa kura wagombea wa CCM.

Nyamahanga amesema, kuna changamoto zilizobakia kidogo kama kukosekana kwa maji kwa baadi ya maeneo, umeme na miundombinu ambapo suluhisho lake ni kukipa kura nyingi Chama Cha Mapinduzi ili viongozi waje wazitatue kero hizo.

Katika jimbo hilo la mafinga madiwani wa kata tano wamepita bila kupingwa huku madiwani wanne ndio ambao wanaenda kugombea katika kata huku mwenyekiti wa CCM mkoa akisema madiwani watano kupita bila kupingwa ni imani kubwa ya watu walionayo kwenye Chama hicho.