Na Heri Shaaban (Ilala)
CHAMA cha Mapinduzi CCM Kata ya Vingunguti wilayani Ilala wanaendelea kubomoa ngome ya Chama cha Wananchi CUF kwa kuvuna wanachama wapya 70 wamejiunga ccm kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za utekelezaji wa Ilani.
Wanachama hao 70 walijiunga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Vingunguti mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM wilaya Ilala Said Sidde, aliyepokea wanachama wapya ndani ya chama hicho ambapo walikabidhi kadi na kupewa kadi za ccm.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Vingunguti Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanachama hao 70 kwa uwamuzi wao kujiunga CCM kuunga mkono juhudi za Dkt samia. Kwa ajili ya kuleta maendeleo.
“Nawapongeza wanachama hawa 70 kujiunga CCM Vingunguti sasa hivi kuna maendeleo makubwa yamefanywa na Chama cha Mapinduzi katika utekelezaji wa Ilani ikiwemo sekta ya afya ,sekta ya Elimu, na miradi mkakati ukiwemo machinjio ya Vingunguti yote haya yamefanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan chini ya wasimamizi wake Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli na Meya omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata hiyo “alisema Sidde
Mwenyekiti Sidde alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,na Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto kwa namna wanavyopambana kuleta maendeleo ya kata hiyo na jimbo kwa ujumla.
Wakati huo huo alitumia fursa hiyo kuwaomba Wananchi wa Vingunguti na wilaya ya Ilala kwa ujumla ,wajitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika Daftari la maboresho ya mpiga kura mwezi Machi,ili watimize haki yao ya msingi kikatiba kwa kupiga kura kuchagua viongozi wanaotokana na chama cha Mapinduzi.
Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto alipongeza wanachama hao kurudi chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo ndani ya chama na Serikal .
Katibu wa ccm kata ya Vingunguti Agata Limbumba alisema Chama cha Mapinduzi CCM Vingunguti wamejipanga kushika dola CCM Vingunguti itaibuka kidede .
Kula za Rais, Ubunge na Udiwani.
More Stories
Madiwani waomba Jimbo la Korogwe Vijijini ligawanywe
Dkt.Nchimbi:Watoa rushwa hawatakiwi CCM
Dkt.Diallo:Nunueni pembejeo mapema baada ya kuuza mazao