Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mmoja tu hivyo kimewataka baadhi ya wanachama na ambao sio wanachama wa chama hicho kuacha,usaliti,uzandiki, majungu,fitna na roho mbaya badala yake wamuheshimu.
Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma leo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma,Dk. Damas Mukkasa kuhusu kumpongeza Rais kwa hotuba yake aliyoitoa Januari 4 Jijini Dare-es-Salaam baada ya kupokea taarifa ya Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko19
“kufuatia alichokizungumza jana Rais Samia Suluhu Hassan na kudai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wamekuwa wakimsaliti katika suala la Nchi kukopa ambapo amesema lazima nchi ikope kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwakuwa fedha za tozo haziwezi kutekeleza mahitaji ya miradi hiyo na kusema mkopo ambao Serikali umeupata wa Sh trilioni 1.3 ni mzuri na haujawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru, sisi tunamuunga mkono Rais wetu na tunampongeza kwa hotuba yake iliyosisimua wananchi ,”amesema Dk.Mukkasa
Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma amemwomba Rais Samia kufanya kazi bila woga na kuachana na baadhi ya watu ambao wana uchu wa madaraka.
Pia,Dk Mukassa ametoa wito kwa Wanaccm kuacha majungu,fitina na roho mbaya, kuacha kuharibiana kwani Rais ni mmoja na hivyo aheshimiwe.
Katika hatua nyingine amelaani makundi yanayowania Urais kwa mwaka 2025 kwani huo ni usaliti na tamaa na badala yake wamuunge mkono Rais katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo katika nchi.
More Stories
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja
Gavu aanika miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita Geita
RC Makongoro: Samia aungwe mkono nishati safi ya kupikia