December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM Mbeya kulinda heshima ya Dkt.Tulia

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

MJUMBE Halmashauri Kuu CCM Taifa (M-NEC)Mkoa wa Mbeya ,Ndele Mwaselela amesema wataendelea kulinda heshima ya Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge,DktTulia Ackson na hawatakubali kuchonganishwa.

Mwaselela ametoa kauli jana Julai 28,2024 wakati wa hafla ya kukabidhi nyumba za wahitaji wawili ambao ni Daines Mbwiga,Solo Mwantengule wakazi wa Kata ya Isyesye sambamba na viti mwendo viwili kwa walemavu.

Nyumba hizo zimejengwa na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson.

“Kama Chama hatufanyi majaribio wala hakitathubutu kufanya majaribio, hatuna mpango tuna msimamo ,binafsi nasema siku zote na hakuna mtu wa kunibadilisha lazima tulinde heshima ya Mkoa “amesema.

Amesema CCM hawana habari ya kuondoa heshima ya Dkt.Tulia na hawatakubali chama kichonganishwe kwa kuondoa heshima ya nafasi Mbunge wa IPU kwa Nyanda za juu kusini .

“Sisi ndo wazazi wa Dkte.Tulia kung’aa kwake kwa ndio chama cha mapinduzi kinazidi kung’aa hivyo asitokee mtu hata kwa kupapasa awe ndani yetu awe nje yetu huyo atakuwa halali yetu ,CCM mkoa wa Mbeya tumebahatika kupata Mhimili mmoja hivyo ni lazima tuulinde”amesema Mwaselela.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Isyesye Jijini Mbeya, Mbunge wa Jimbo la Mbeya na Spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani,Dkt.Tulia Ackson amesema kuwa mpaka Sasa ameweza kujenga nyumba 16 za wahitaji ambapo kati ya hizo mbili zimejengwa nje ya Mbeya.

Dkt amesema kuwa nyumba zilizokabidhiwa leo ambazo ni za wananchi wawili ambao walikuwa wakiishi katika mazingira magumu kwa kukosa makazi rasmi .

Meya wa Jiji la Mbeya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Isanga ,DorMohamed amesema kuwa Dkt ni Mbunge makini na mnyenyekevu kwani ameleta mkurugenzi wa Jiji anayejitambua na kusimamia vema miradi yote ya maendeleo kikamilifu.

“Ndugu zangu wananchi msiruhusi sisimizi kuingia kwenye baraza la madiwani, tufanye kazi kwa uaminifu na kumsemea mazuri aliyofanya Dkt Tulia hii tunu hatupaswi kuipoteza kamwe “amesema Meya huyo .