Na Yusuph Mussa, Timesmajira Online,Lushoto
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lushoto kimempongeza Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kupeleka gari lenye mtambo wa kuchimba visima ikiwa ni jitihada za kumaliza kero ya maji kwa kata na vijiji ambavyo havina vyanzo vya uhakika wa maji ya mserereko.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto Ali Daffa amesema kwenye ziara ya siku nne aliyoifanya Lushoto kuanzia Januari 6 hadi 9, mwaka huu, Mahundi alionesha kuguswa na adha ya kukosa maji wanayokumbana nayo wananchi, na kuahidi kuleta gari la kuchimba visima.
“Hivi karibuni Mhandisi Mahindi alitembelea Wilaya ya Lushoto na moja ya ahadi yake ni mitambo hii kufika Lushoto Januari 14, ahadi hiyo imetimia baada ya mtambo kufika kama Naibu Waziri alivyoelekeza, tunampongeza kwa hilo. Kwa maana hiyo serikali ya Chama Cha Mapinduzi inapoahidi jambo linatekelezwa,”amesema Daffa.
Daffa amesema baada ya mtambo huo kufika, kazi iliyopo ni wataalamu kuhakikisha visima vinaanza kuchimbwa ili wananchi wapate maji huku akitoa wito kwa wataalamu hao kufanya kazi kwa weledi ili maji ya
“Najua maeneo mengi yanauhitaji, hivyo kazi ya kupanga kisima kichimbwe wapi, na kuanzia wapi,ni kazi ya kitaalamu isije ikaanza mivutano ya tuanze hapa, tuanze hapa… hapana,tuwaachie wataalamu wetu ambao wataamua wachimbe wapi na wapi, na mwisho wa siku maeneo yaliyokusudiwa kupata visima yawe yamepata,”amesema Daffa.
Daffa amesema wataalamu wameahidi kuwa shida ya maji itakuwa historia, lakini baada ya kupata maji hayo, wananchi wanatakiwa wachangie ili miradi ya maji iwe endelevu anaamini gharama ya maji hayo ni ndogo kuliko gharama ya kuyafuata maji mbali na wakati mwingine hawayapati.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Januari 18, 2024 ofisini kwake, Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Lushoto Mhandisi Erwin Sizinga amesema gari hilo la mtambo wa kuchimba visima limefika Lushoto Januari 15, mwaka huu na wakati wowote kuanzia sasa, linakwenda vijijini kuanza kazi.
“Gari tumelipokea sasa tunaweka mipango sawa ili kuweza kuanza kazi. Wakati wowote litakwenda vijijini kuanza kazi. Tunawaahidi wananchi tutafanya kazi hii kwa weledi ili kuona wananchi wanapata maji ya uhakika na salama,”amesema Mhandisi Sizinga.
More Stories
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki