March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM kutatua kero za wananchi kwa kutumia kliniki kwenye ziara

Na Zena Mohamed,TimesmajiraOnline,Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kuanza ziara kueleza mikakati pamoja na kuanzisha kliniki ya kisiasa kwa kufanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo ambayo iliahidiwa na chama hicho katika uchaguzi Mkuu 2025

Hayo yamesemwa jijiji hapa leo Januari 17 ,2026 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Kenani Kihongosi wakati akizungumza na waandishi wa habari  juu ya uanzishwaji wa ziara za kukagua miradi iliyoahidiwa na Serikali inayotarajiwa kuanza kesho 18 Januari 2026. 

Kihongosi amesema kuanzia Januari 18 mwaka huu ataanza ziara ya kichama itakayohusisha mikoa yote ya Tanzania huku akieleza kuanzia Mkoani Singida na wilaya zake ambapo ziara hiyo inalenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi kuimarisha chama na kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Rais Samia

” Ziara hii ni jukwaa la wananchi kama kuna anayehisi kuonewa au kunyanyaswa tunawakaribisha waje ili tusikilize na kutatua changamoto zao, “Kihongosi 

Kihongosi pia ametoa pongezi kwa Rais Samia kwa kukutana na Mabalozi wa Tanzania Januari 15 2026 katika kikao cha ufunguzi wa mwaka akisema mkutano huo umeimarisha hadhi ya Tanzania kimataifa na kuonesha mwelekeo chanya wa diplomasia ya nchi. 

Pia ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa kodi ambapo makusanyo yamefikia shilingi trilioni 3 1 na mwezi Desemba kuvuka zaidi ya shilingi trilioni nne .

Kuhusu masuala ya kijamii Kihongosi amesema Serikali inaendelea na maandalizi ya uzinduzi wa bima ya afya kwa wote huku ikichukua hatua za kuondoa tabia ya kuzuia maiti kwa wagonjwa wasiolipa gharama za matibabu. 

Aidha ameeleza kuwa Serikali imetekeleza ahadi ya ajira kwa kutoa ajira zaidi ya 12 000 katika sekta mbalimbali na mpango wa kutoa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha vijana bado unaendelea.

Hata hivyo katika mkutano akijibu swali na Mwandishi kuhusu Jaji Warioba kuonekana mitandaoni akitoankauli za malalamikonlicha ya kukutana na  Rais Samia chama  hicho kimesema  Jaji Mstaafu Joseph Warioba kwa mtaka kuacha chuki kwa viongozi wa Serikali.

Kihongosi  akimzungumzia mwanasiasa nguli  huyo Jaji Warioba amesema umefika sasa wakati wake wa kutulia ili astaafu vizuri na aache kulalamika na kutoa kauli tata na pia aache wivu kwa viongozi wa Serikali.

Kihongosi amesema CCM ni chama kinachojengwa juu ya misingi ya maridhiano umoja na kuheshimiana hivyo hakitovumilia juhudi zozote za kupotosha ukweli au kueneza chuki zisizo na tija kwa Taifa. 

Amesema CCM inamheshimu Waziri Mkuu na Jaji Mkuu Mstaafu Joseph Warioba kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa lakini ikamtaka kuendelea kufurahia maisha ya kustaafu kwa utulivu bila kutoa malalamiko. 

“Ni jambo la kawaida kwa viongozi waliotumikia Taifa kuheshimiwa lakini wastaafu wanapaswa kutoa nafasi kwa viongozi waliopo kuendelea na majukumu yao Kihongosi, “amesema

Nakuongeza kuwa “Licha ya Jaji Warioba kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan bado alionekana mitandaoni akitoa kauli zenye malalamiko hali aliyoitaja kuwa haina tija kwa maendeleo ya Taifa, “. Amesema