Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Geita
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, endapo kitapewa tena ridhaa ya kuongoza nchi, moja ya mpango mkakati itakayofanya ni kuimarisha sekta ya madini mkoani Geita.
Hayo yamesema Septemba 6, 2025 na Mgombea Mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano mdogo uliofanyika Kata ya Katoro mkoani Geita, akiwa kwenye muendelezo wa kampeni za kukinadi chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Dkt.Nchimbi amesema, Serikali chini ya CCM endapo itaendelea kushika dola, itaimarisha zaidi sekta ya madini ikiwa ni pamoja na kuongeza utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo na kipaumbele kwa vijana wa kitanzania kuwekeza katika madini.
Pia itajenga hospitali 10, vituo vya afya 61, zahanati 271, shule za msingi 770, madarasa 22,716, kuongeza mradi wa mtandao wa maji safi na salama, kuongeza skimu ya umwagiliaji na ruzuku ya mbolea na upatikanaji wa umeme katika vitongoji vyote vya Mkoa wa Geita.

Dkt Nchimbi anaendelea na mikutano yake ya kampeni mkoani humo kusaka kura za ushindi wa kishindo wa (CCM), akitokea mkoani Shinyanga.
Aidha mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa jimbo la Katoro, Dkt Nchimbi aliwanadi wagombea Ubunge, akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Katoro, Mhandisi Kija Ntemi pamoja na Madiwani.




More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani