Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Simiyu
MGOMBEA Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo endapo chama hicho kitashinda katika uchaguzi mkuu kitahuisha mchakato wa Katiba mpya.

Dkt.Nchimbi ametoa kauli hiyo Septemba Mosi 2025,Kata ya Dutwa mkoani Simiyu, ikiwa muendelezo wa kampeni ya chama hicho kwa ajili ya kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.
Amesema sambamba na mpango huo CCM imedhamiria ndani ya miaka mitano ijayo itaendelea kusimamia na kudumisha amani kwa Watanzania.


More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama