Na Zena Mohamed,TimesMajiraOnline,Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema ili kuboresha uchumi kwenye chama hicho kunahitaji uwekezaji hivyo amezitaka ngazi zote za chama hicho kutoka shina, tawi, kata, wilaya,Mkoa na Makao Makuu kuwekeza kwenye uchumi ili zijiendeshe badala ya kutegemea hisani.
Chongolo amesema hayo jijini hapa leo katika Kongamano la Mafunzo ya Uongozi na uwajibikaji katika mada za Itikadi,Elimu ya Sensa na makazi,Tehama na Usajili wa Wanachama pamoja na Masuala ya Ulinzi na Usalama kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi za Mashina.
Ambapo amesema uboreshwaji wa uchumi kwenye chama itasaidia mambo yote kuwa rahisi na wataepuka kukimbiana katika vikao vya kujenga masuala yote ya msingi.
”Ni lazima kwanza tuboresha uchumi ili mambo yatunyookee, tukiboresha uchumi wa chama chetu mambo yetu yote yatakuwa rahisi na tutaacha kukimbiana kwenye masuala ya Msingi na hivi karibuni tutakusanya mikoa ambayo imelala lala tunawachukua waje kujifunza waone Mikoa mingine inavyofanya vizuri Mkoa wa Dodoma ni moja kati ya Mikoa inayofanya vizuri katika suala la Uchumi,”amesema Chongolo
Hata hivyo amewataka wagombea wanafasi mbalimbali wa chama hicho kuepuka vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha uchaguzi ikiwi ni kiapo cha Mwanachama ambayo ni ahadi katika chama.
“Tunaposoma ahadi ya Mwanachama kila mmoja aliapa kuwa rushwa ni adui wa haki na pale mlikuwa mkimaanisha kuwa rushwa ni jambo lisilokubalika,kila Mmoja atumie yale mema yake ambayo anaona ataweza kujinadi,
“Tufanye Kampeni kwa kutumia nguvu zetu bila kutengenezeana uongo na uzushi pamoja na kutengenezeana ajali tusipende kuwekeana chuki sisi kwa sisi,”amesema.
Hata hivyo Chongolo ameagiza vikao vitakavyo jadili majina ya wahusika katika ngazi usika kutoona aibu kuchukua hatua kwa watu watakao kiuka maagizo halali yaliyowekwa na Chama.
“Hatuwezi kuwa chama ambacho tunatoa maelekezo kwaajili ya kutoa fursa kwa Watu wote kuwa sawa kwenye kugombania kinyang’anyiro cha kugombea nafasi mbali mbali na baadhi ya wachache kuona wao wanapembe ndefu kuliko Mmiliki wa pembe usika,
“Chama ndicho chenye dhamana na nafasi, Mtu ukiona unataka dhamana hiyo usipo fuata maagizo na maelekezo yetu utakuwa hututakii jambo zuri na utakuwa unatulazimisha kuchukua hatua na hatutosita kuchukua kwasababu utakuwa ameyataka mwenyewe,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema mafunzo hayo kwa viongozi wa mashina na matawi ni muhimu kwasababu wao ndio wanaojua wananchi wanaowaongoza moja kwa moja.
Hivyo amewaasa kuwa mafunzo watakayoyapata yakawasaidie kuhamasisha watu kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi pamoja na kuhamasisha suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi.
Amesema kuwa viongozi hao ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi kwasababu wanakumbana na shida za wananchi moja kwa moja.
“Tunaomba mkatusaidie sana katika suala la ulinzi na usalama katika maeneo yenu ya kazi msikubali kuona watu wanakuja katika maeneo yenu na kuishi bila ninyi kupata taarifa naamini baada ya mafunzo haya mtaleta mageuzi hasa katika kuhamasisha wananchi kujilinda na kujitokezakwa wingi katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu,”amesema.
More Stories
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi