Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
CHAMA cha Mapunduzi CCM Kata ya Kipawa Wilayani Ilala,imewataka wana ccm wa Kata ya Kipawa wasijaribu Kunywa sumu wakatawaliwa na UKAWA kwani sumu aijaribiwi .
Hayo yalisemwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kipawa Jafari Napinda Nambunga, wakati wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya kata ya Kipawa Albert Otieno Mgoe , alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama kwa 2023 Hadi 2024 Juni .
“Wana ccm sumu aijaribiwi hivyo hivyo msikubali kunywa sumu mkatawaliwa na vyama vya upinzani UKAWA badala yake nawaomba muungane muwe wa moja kuakikisha ccm inashika dola inapanga Serikali yake.”alisema Namunga.
Katibu wa ccm Kipawa Namunga alisema kuongozwa kwa ccm ni Faraja kubwa maendeleo katika Mtaa wetu ,katika kata yetu ya Kipawa JIMBO letu la segerea kutokana na viongozi waliopo madarakani kushirikiana pamoja katika kuleta maendeleo hivyo wadumishe umoja na mshikamano katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Aidha aliwamasisha wa kajiandikishe katika Daftari la mpiga kura Mwezi Julai mwaka huu zoezi hilo litakapoanza Rasmi ili waweze kupata haki ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwani kupiga kura ni haki ya kila mmoja .
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kipawa SAID MKUWA alimpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji Mpya Albert Otieno kwa utendaji wake wa kazi na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani vizuri .
Mwenyekiti SAID MKUWA aliwataka Kipawa kuwa wamoja kwa kushirikiana na Wajumbe wa Mashina na chama pia aliwataka Wajumbe wa mashina waitishe vikao na kuwasilisha taarifa za kero za wananchi ngazi ya chama kwa ajili ya utatuzi wake.
Wakati huo huo Mwenyekiti SAID MKUWA alipiga Marufuku wana CCM kipawa wasikwamishe Maendeleo ya Serikali Mwana ccm atakaye kwamisha Maendeleo achukuliwe hatua ndani ya chama..
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato