Na Mwandishi Wetu, Timesmajiraonline
KATIBU wa Halmashauri Kuu NEC ya Chama Cha Mapinduzi CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amoss Makalla amesema ushindi wa Chama hicho unatokana na imani ya wananchi inayotokana na kazi nzuri ambazo zimefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo nchini kote.
CPA Makalla alisema hayo jana jijini Dar es Salaam akiwa katika mwendelezo wa kampeni zake za uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu na kueleza kwamba Rais Samia amefanya maendeleo makubwa ya yanayoonekana kwa uwazi.
Akiwa katika Jimbo la Ukonga, Makalla alieleza hatua kwa hatua kuhusu maendeleo ambayo Rais Samia aliyafanya nchini na mazuri hayo ndio yanayowapa matumaini kwa wagombea wa CCM kushinda kwa kishindo.
“CCM inabebwa na kazi nzuri zinazofanywa na wabunge na madiwani wake, hivyo tunaimani CCM inauzwa na kazi nzuri iliyofanywa na waheshimiwa wabunge, madiwani na Rais, kwani kazi zake zinaonekana,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa CCM wanatembea kifua mbele kwa ajili ya kiongozi wao ambaye ni mwenyekiti kitaifa Rais Samia Suluhu Hassan na 4R zake na fedha anazozitoa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
CPA Makalla amefafanua kuwa yote ambayo wapinzani walikuwa wakiyapigia kelele Rais Samia ameyafanyia kazi,hivyo wapinzani katika kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka huu wamekosa hoja za kuwaambia wananchi na tayari wameshakubali kushindwa katika uchaguzi huo.
“Wapinzani wamekosa haja za kueleza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwasababu Rais DK.Samia Suluhu Hassan amewafilisi. Kimsingi Rais Samia amegusa yote ambayo wapinzani walikuwa wanayalalamikia.Leo hawana cha kuwaambia Watanzania.”
Alisema chini ya uongozi wa Rais Samia kampeni wanafanya kampeni zake kwa kutuata R4 ,hivyo kampeni zao zitakuwa za kistaarabu na hawatamkejeli mtu kwani kuna maendeleo mengi yakuelezea ambayo Rais ameyafanya katika maeneo mbalimbali nchini.
“Wana CCM wanatembea kifua mbele kwasababu ya mambo makubwa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya nchini kwetu,”alisema na kusisitiza kwa maendeleo ambayo Rais aliyafanya kuna idadi kubwa ya wagombea wa vyama vya upinzani wako katika orodha ya wanaotaka kurudi CCM”
“Kila mahali Rais Samia alipeleka fedha , alitekeleza miradi na ndio maana leo katika mkutano huu tunaye kiongozi wa kitaifa waTLP ameamua kuja kuungana na Wana CCM kuomba wananchi wachague wagombea wa CCM.”
Pamoja na hayo alisema wakati viongozi wa CCM wakiwatumikia Watanzania katika kuleta maendeleo vyama vya upinzani hasa CHADEMA wao walikuwa wakihamasisha maandamano na kimsingi maandamano hayo yamewasaidia zaidi kupata fedha lakini wanachama wao wakifanyishw mazoezi yasiyo na faida kwao wala kwa Taifa.
Hivyo alisema kuna kila sababu ya kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa Chama hicho na kusisitiza Chama hicho hakihitaji mbeleko kwasababu kwa mambo yaliyofanywa na Rais Samia, Wabunge na Madiwani wanauhakika wa kushinda.
“Tutashinda kwasababu yaliyofanywa na Rais Samia yanatufanya tuwe na imani na ushindi wa kishindo.Kazi zetu ndizo zinatupa ushindi,”amesema na kusisitiza kwa sasa wabunge na madiwani wengi ni wa CCM hivyo hata alipatikana mgombea wa upinzani anakwenda kufanya kazi na nani.
Akielezea zaidi katika mikutano ya kampeni anayoendelea kuifanya CPA Makalla amemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akisema kuwa wagombea wao ni waaminifu lakini ukweli Chama hicho hawana uaminifu wowote huku akikumbusha Wabunge 19 wa Chama hicho waliofukuzwa na kuwaita COVID-19 .
“CHADEMA hawaamini kabisa na mnakumbuka waliwafukuza Wabunge wao 19 na wakaanza kuwaita majna mabaya,lakini Wabunge hao walikwenda mahakamani wakishinda kesi na sasa wanachukua ruzuku.
“Sasa la kujiuliza kama waliwafukuza Wabunge wao mnaujakika gani wakipata wagombea katika Serikali za Mitaa hawatawafukuza? Ndio maana nawaomba Watanzania msipoteze muda na wapinzani hawaamini lakini hata Ilani hawa a zaidi kuwa wanabuni na kufikiria kutoka katika vichwa vyao,”amesema CPA Makalla.
Kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji zinatarajia kumalizika Novemba 26 mwaka huu lakini CCM imejiridhisha kuwa itashinda uchaguzi huo kwani wagombea wao wanazo sifa zote na wamechujwa na vikao vya Chama.
Aliwakumbusha umuhimu wa Wana CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27 mwaka huu ili kuhakikisha wagombea wa Chama hicho wanashinda kwa kishindo na kufafanua katika uchaguzi huo kutakuwa na kura ya ndio na hapana,hivyo ili kuwa na uhakika wa kura .
“Twendeni tukapige kura ili tushinde kwa kishindo,tushinde ushindi wa heshima.Asitokee mtu wa kuwadanganya kuwa katika Mitaa ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea usiende kupiga kura.Wote tukapige kura ya ndio kuhakikisha ushindi unakuwa wa kishindo.”
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024