February 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM imedhamiria kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi

Na Mwandsihi wetu,Timesmajira

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimedhamiria kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi kwa kuendelea kuwatoa katika hali duni na kuwajengea misingi ya maisha bora kwa kadiri inavyowezekana.

CCM imesema ukilinganisha na miaka 60 iliyopita Watanzania wa sasa wana hali bora Zaidi kutokana na kuimarika kwa maisha katika sekta mbali ikiwemo ya elimu na huduma za jamii.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyrkiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akizungumza na wana-CCM alipowasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Tarime.

“Tunataka kufanya mapinduzi ya maisha ya watu na tunafanya, ndiyo maana watu wa Tarime sasa ni watu tofauti na waliokuwepo miaka 60 iliyopita. Unasimama unasema hatujafanya kitu, tumefanya, tumesomesha watu wengi sana hata wanaosema hatujafanya chochote tumewasomesha na uhuru wa kusema hatujafanya chochote tumewapa.

Amesema katika kipindi cha miaka minne pekee ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan serikali imeleta mabadiliko makubwa nchini ikiwemo wilayani Tarime ambako imejenga madarasa bila ya kuwachangisha wananchi kama ambavyo ilikuwa ikifanyika awali.