April 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM hakuna mgombea kupita bila kupingwa

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimefanya mabadiliko katika mchakato wa upatikanaji wa wagombea ndani ya chama hicho, kuelekea uchaguzi mkuu,ambao watapigiwa kura za ndiyo au hapa,hivyo hakutakuwa na kupita bila kupingwa.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA. Amos Makalla, ameelezea hayo Machi 7,2025,katika mkutano wa ndani wa chama hicho na wakati akizungumza na viongozi wa chama ngazi ya tawi, kata na Wilaya, wilayani Temeke jijini Dar-es-Salaam, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tano mkoani humo.

Makalla amesema CCM imefanya marekebisho mawili, ikiwemo uchujaji wa wagombea kabla ya kura za maoni tofauti na ilivyokuwa hapo awali, ambapo lilikuwa likirudi jina moja na kupitishwa bila kupingwa, hivyo amewaambia Wabunge na Madiwani kutakuwa na usalama na utulivu pamoja na suala la kupitia bila kupingwa halipo.

Pia amesema,awali watu walikuwa wanachukua fomu na kurudisha jina moja,lakini utafanyika mchujo wa awali kwa kurudisha majina matatu ambayo yatapigiwa kura za ndiyo au hapana.