Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza
BWENI la Shule ya Sekondari ya Wasichana Loreto iliyopo wilayani Ilemela limeteketea kwa moto, huku wanafunzi zaidi 100 wakinusurika katika tukio hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Severine Lalika, amesema kwamba wamepokea kwa masikitiko tukio hilo, huku akihimiza shule zote za bweni na taasisi zinazohudumia wananchi kujenga kwa mabweni kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa zimamoto na uokoaji ili kuepusha majanga ya moto yanayojitokeza.
Dkt.Lalika ametoa wito huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, wakati wa ibada ya shukrani ya kuwaombea wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukubwa na ajali hiyo ya moto.
Amesema ni muhimu kuzingatia maelekezo ya zimamoto na uokoaji kila kila jengo la bweni liwe na miundombinu inayokidhi mahitaji pamoja na vifaa vya kudhibiti majanga ya moto.
Amesema,chanzo cha moto katika bweni hilo la ghorofa ya tatu ni shoti ya umeme. Alisema chanzo hicho cha moto kimethibitishwa na wataalamu wa TANESCO, Polisi na Zimamoto baada ya kufanya uchunguzi.
“Hivyo naishauri shule hiyo na shule nyingine kuhakikisha miundombinu ya umeme katika majengo yao kila wakati inakuwa salama ili kuhakikisha hakuna matukio kama hayo,”amesema.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sister Basilisa Matem,amesema wanashukuru Serikali kuwa pamoja nao na wanamshukuru Mungu kuwa watoto wapo hai hakuna aliyepoteza maisha.
Bweni lililoungua lina uwezo wa kukaa zaidi ya wanafunzi 500, lakini wakati wa tukio hilo bweni lilikuwa na wanafunzi zaidi ya wanafunzi 100.
Amesema bweni hilo liliungua majira ya saa 12.20 jioni na kwamba vitu vyote katika bweni lililoungua viliteketea, hivyo amewaomba wazazi watulie kwani watoto wapo salama.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angeline Mabula, amesema matukio kama hayo mara nyingi yanaumiza watoto
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi