LONDON, Waziri wa Afya wa Uingereza, Matt Hancock amejiuzulu baada ya kuvunja sheria ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19).
Ni sheria ambayo inataka kila mmoja kuweka umbali wa mtu mmoja hadi mwingine ambapo yeye na msaidizi wake mkuu, Gina Coladangelo wanadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Gazeti la The Sun lilichapisha picha zilizoonekana zikimuonesha Hancock na Coladangelo wakibusiana katika ofisi moja ya wizara hiyo ya afya.
Katika barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, Hancock alisema kuwa serikali ina wajibu kwa watu wake ambao wamejitolea zaidi katika janga la virusi vya corona na kuwa waaminifu kwao wakati imewakosea.
Hancock aliongeza kuwa, anataka kusisitiza ombi lake la msamaha kwa kuvunja muongozo na kuiomba radhi familia na wapendwa wake kwa tukio hilo na kwamba anahitaji kuwa na watoto wake kwa wakati huu.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi