Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Tanga
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exhaud Kigahe ameziagiza BRELA, SIDO na taasisi husika kufika katika gazi za Halmashauri ili kuwawezesha wafanyabiashara kwani serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
Amesema hayo Octoba 3,2023 wakati akifunga kongamano la Biashara na Uwekezaji wilayani Pangani jijini Tanga lililofanikiwa kuwakutanisha wafanyabishara mbalimbali mkoani humo.
Ambapo ameeleza kuwa serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuhakikisha sekta binafsi zinafanya vizuri katika maendeleo ya biashara na uchumi hivyo taasisi hizo zinapaswa kufika maeneo hayo ili kuwezesha kundi hilo.
Aidha amewataka wafanyabiashara,wadau wa maendeleo na wajasiriamali kuchangamkia fursa za utalii, kilimo, ufugaji na uchumi wa bluu katika Wilaya ya Pangani.
Kigahe amesema ni wakati sasa thamani ya malighafi nchini iongezeke iwe maradufu na nchi iwe inazalisha bidhaa zilizokamilika ili ziweze kuingia katika soko huru la biashara Afrika na masoko mengine ndani na nje ya Afrika
Naye Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Issah ameishukuru serikali kwa kuwapeleka maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo, Daraja la mto Pangani na miradi mbalimbali ili kuweza kuhamasisha uwekezaji na muingiliano wakibiashara ndani na nje ya nchi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba