Na Penina Malundo,Dar es Salaam
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA),imesema kuwa kutokana na Kilimo kuwa biashara wakulima wanapaswa kurasimisha biashara zao ili waweze kufanya biashara kwa urahisi zaidi.
Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano BRELA, Roida Andusamile wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Mifumo ya Chakula (AGRF 2023) unaoendelea jijini Dar es Salaam amesema kutokana na wakulima kuwa miongoni mwa wadau wakubwa wanapaswa kurasimisha biashara zao.
Amesema kwa sasa BRELA usajili wake unafanywa kwa njia ya mtandao na sio analogia hivyo huduma zao zote wanazitoa kwa njia ya kidigitali na kama kuna changamoto yoyote kwenye mfumo wanamuhudumia mteja papo kwa hapo.
“Tunawakaribisha watu mbalimbali waliofika Mkutano AGRF 2023 kufika katika banda letu ili kuweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo kufanya usajili wa majina ya biashara zao,”amesema na kuongeza
“Tunatoa usaidizi wa usajili wa majina ya biashara, kampuni, alama za biashara na huduma pamoja na utoaji wa leseni za biashara kundi A na za viwanda,”amesema.
Amesema muda uliyobakia wa Mkutano huo,wanawakaribisha wadau wao kufika katika banda lao ili wapate huduma hizo za Brela kwa urahisi zaidi.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja