Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
WAKALA wa Usajili wa Biashara na utoaji wa Leseni za viwanda (BRELA) imewataka wafanyabiashara wote nchini kusajili majina ya biashara,majina ya kampuni kabla ya kuanza Biashara ili kuepuka jina la biashara kuchukuliwa na kubadilisha taarifa upya.
Akizungumza kwenye maonyesho ya 9 ya biashara na utalii jijini Tanga,Msajili msaidizi Idara ya Makampuni na Biashara kutoka BRELA, Selemani Selemani amesema ni vema wafanyabiashara wakajitokeza kusajili biashara zao.
Aidha Seleman alisema wapo kwajili ya kusaidia jamii ili waweze kufanya biashara zao bila kuwa na kikwazo chochote hivyo wanapaswa kuipa umuhimu biashara yao kwa kuisajili Brela.
“Nitoe wito wetu sisi BRELA tunawahamasisha watu wasifanye biashara kibubu,unaposajili biashara yako inatambulika kisheria hivyo kuifanya biashara yako haiwezi kuchukuliwa na mtu yeyote”alisema Selemani
Ameongeza kuwa ni vema biashara kuisajili ili isiweze kutumika popote,na ni muhimu kabla ya kuanza biashara ni vizuri kufanya usajili biashara ili isilete mkanganyiko
“Wito wangu kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa kabla ya kuanza kutumia majina kwenye biashara zao wahakikishe kwanza wamesajili Brela,unaposajili BRELA inakua umelikinga jina lako kutumika kwingine”alisema Selemani
Kutokusajili jina la Biashara na ikawa kubwa inaweza kuleta changamoto pindi utakapotaka kusajili,na utakapolikuta lipo itakulazimu kubadilisha taarifa yote ya biashara unayoifanya.
More Stories
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji