December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA yashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania kwasababu ni Maonesho yanayohusu Viwanda na Bidhaa zake hivyo BRELA kwa majukumu yake kisheria inatumia fursa ya Maonesho hayo kuhamasisha wenye viwanda kusajili alama za biashara na huduma ili kulinda umiliki wa alama zao.

Pia BRELA imelenga kuwahamasisha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao ili wajulikane katika Sekta.

Gaston Canuty akipata usaidizi wa karibu wa namna ya kufanya mabadiliko ya taarifa ya kampuni kutoka kwa Paul Peter Afisa kutoka Brela. BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.
Davide Firno mwekezaji nchini Tanzania akipata elimu na usaidizi wa sajili kutoka BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.
Issa Ally Njoka mzalishaji wa bidhaa ya Lishe akipata elimu ya Alama ya Biashara juu ya bidhaa anayozalisha kutoka kwa Bw Raphael Mtalima Afisa Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Haki Miliki. BRELA inashiriki Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Baraka Mwakyalika akikabidhiwa Cheti cha Usajili kutoka Afisa wa BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Zanzibar wakipata elimu ya namna BRELA inavyotekeleza majukumu yake walipotembelea banda la BRELA kwenye Maonesho ya Sita ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika Zanzibar katika Uwanja wa Maisara