March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA yashinda tuzo, Kundi Bora la Uwezeshaji Biashara na Uwekezaji

Na Penina Malundo,Timesmajira

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshinda tuzo ya Kundi Bora la Uwezeshaji Biashara na Uwekezaji katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba. Ushindi huu ni ushahidi tosha wa

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bwana Seka Kasera, Meneja wa Sehemu ya Alama za Biashara na Huduma, aliwapongeza kwa dhati watumishi wote wa BRELA kwa juhudi na weledi waliouonesha wakati wote wa maandalizi na ushiriki kwenye maonesho hayo.

Aidha, alitoa shukrani kwa wadau mbalimbali wa BRELA ambao wameendelea kutumia mifumo ya mtandao kusajili biashara, kampuni, alama za biashara na kupata leseni, akisema kuwa wao ndio chachu ya mafanikio ya taasisi hiyo. “Mshikamano huu kati ya BRELA na wadau ndio msingi wa mafanikio tunayoyaona leo,” alisisitiza.

Katika kipindi chote cha maonesho, BRELA ilitoa Huduma za papo kwa papo zinazopatikana kwa njia ya mtandao, jambo lililowavutia wadau mbalimbali. Mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao ORS umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza urasimu, kuongeza ufanisi na kuwezesha wananchi wengi zaidi kuanzisha biashara kwa urahisi na haraka.