January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA yajidhatiti kutoa huduma Bora Kwa wateja wake

Na David John timesmajira online Geita

MKUU wa Idara ya Miliki Brela Loy Mhando Amesema Mamlaka hiyo imeongeza nguvu kiutendaji na kuendelea kuhudumia wafanyabishara kwa ufanisi mkubwa bila kuwakwamisha ili waweze kufanya biashara zao bila vikwazo.

Mhando ameyasema hayo septemba 23 mwaka huu katika maonyesho ya teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA vilivyopo eneo la Bombambili mkoani Geita.

“Brela itahakikisha inamfikia kila mfanyabiashara ili aweze kupata huduma kwa wakati na hilo ndio jukumu kubwa la Mamlaka hii .tupo Kwa ajili ya kuwahudumia wananchi “Amesema

Amefafanua kuwa BRELA imepokea kwa mikono miwili maagizo ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ambaye ameagiza taasisi zote zinazo husika na kutoa leseni na kuhudumia wafanyabishara kutowakwamisha wafanyabishara.

Mhando amesema kuwa Brela inatoa huduma zote kwa njia ya mtandao na mfanyabiashara anaweza kuomba huduma akiwa popote alipo bila kulazimika kufika ofisini.

Kwaupande wake Afisa leseni BRELA Jubilate Muro amesema mfanyabiashara ni lazima after kanuni sahihi za leseni ili aweze kufanya biashara kwa uhuru.

Amebainisha brela inamuwezesha mfanyabiashara kutambulika ndani na nje ya nchi ikiwemo na kutambulika katika mabenki na kumrahisishia utendaji rahisi katika biashara zake za kila siku.

Ametanabaisha mfanyabiashara ni lazima afate hatua stahiki katika mfumo wa usajili kwa kutimiza baadhinya vigezo muhimu vikiwemo kuwa na kitambulisho cha utifankutoka NIDA.
Kama ni mbia kutoka kwenye kampuni ni lazima uwe na kitambulisho cha NIDA

Vilevile kama ni mkurugenzi wa kampuni lazima uwe na kitambulisho cha utaifa kutoka NIDA na namba ya utambulisho wa mlipa kodi TIN ya nchi husika.