Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza ongezeko la wagonjwa 14 wa virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19) hapa nchini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (TAARIFA KWA UMMA) kwa sasa hapa nchini kuna wagonjwa 46 kutoka 32 waliotolewa taarifa Aprili 10, mwaka huu. Waziri Ummy amebainisha kuwa, wagonjwa wapya 14 wote ni Watanzania.
Kati ya hao wagonjwa waliopo jijini Dar es Salaam ni 13 na mmoja yupo Arusha. “Wagonjwa wote wanaendelea na matibabu chini ya uangalizi wa wataalam wa afya.
Ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa,” amesema Waziri. Wakati huo huo Serikali imeendelea kusisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kama inavyoendelea kuwapatia elimu kwa kushirikiana na vyombo vya habari. Taarifa zaidi jipatie nakala yako ya Majira…
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya