TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi kama ifuatavyo:
- Amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).
- Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
- Amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.
- Amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
- Amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.
- Amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.
- Amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba
- Amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.
Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua