December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS:Iran jino kwa jino na Marekani, yaagiza Rais Trump, wenzake 30 wakamatwe

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Tehran

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Marekani, Donald Trump na wenzake zaidi ya 30 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani.

Mauaji hayo yalitokea katika shambulio la Januari 3, mwaka huu mjini Baghdad, Iraq. Huku Iran ikitoa wito kwa Interpol kusaidia kufanikisha hilo.

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Jamhuri hiyo, Ali Alqasimehr amesema leo kuwa, Rais Trump na wenzake 30 wanahusishwa moja kwa moja na tukio hilo la mauaji na ugaidi.

Kwa mujibu wa ISNA, Alqasimehr hakuainisha majina ya watu wengine zaidi ya kumtaja Rais Trump ambaye amesema, tuhuma zinazomkabili zitashughulikiwa hata hapo atakapofikia ukomo wa utumishi wa umma kupitia nafasi ya urais.

Aidha, Interpol yenye makao mjini Lyon, Ufaransa haikujibu mara moja ombi hilo la Jamhuri ya Kiislam ya Iran.

Wakati hayo yakijiri, mmoja wa wawakilishi wa Marekani nchini Iran,Brian Hook aliyaeleza madai hayo kuwa ni ya kipropaganda.

“Ukweli ni kwamba Interpol huwa haiingilii mambo ya namna hii ambayo yanaishara ya hati nyekundu,mambo ambayo yana asili ya kisiasa,”amesema Hook katika mkutano na waandishi wa habari nchini Saudi Arabia.