December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Zitto na Bwege wakamatwa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Kilwa

Zitto, Bwege wakamatwa na Polisi

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege) wamekamatwa na Polisi muda huu wakiwa kwenye kikao katika Jimbo la Kilwa Kusini.

Taarifa iliyotolewa hivi punde kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu Uenezi, Habari na Mahusiano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, Janeth Rithe, imethibitishwa kukamatwa kwa Zitto.