Na Mwandishi Wetu
TONGA, Kimbunga kilichopewa jina la Harold kimesababisha maafa mbalimbali vikiwemo vifo vya watu 27 katika visiwa vya Pasifiki.
Kimbunga hicho ambacho kinaelezwa kwenda kwa kasi kubwa kinatajwa kusababisha uharibifu pia katika maeneo ya utalii Kusini mwa Pasifiki.
Aidha, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia
msemaji wake, ametuma salamu zake za rambirambi pamoja na kusikitishwa kwake kutokana na kimbunga Harold ambacho kimezipiga nchi za visiwa vya Pacific na kusababisha vifo na uharibifu wa mali.
Kwa kina zaidi endelea katika Gazeti la Majira…
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya