Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
RAIS wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitalini katika Mji Mkuu nchi hiyo Windhoek.
Kwa mujibu wa tangazo lilitolewa na Makamu wa Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba Geingob ameifariki leo asubuhi.
Makamu wa Rais ameeleza “Pembeni yake alikuwa mke wake mpendwa Madame Monica Geingos na watoto wake,”
Hage mwenye umri wa miaka 82 aliugua saratani ambapo aligundulika baada ya uchunguzi wa matibabu na kuutangazia umma mwezi uliopita.
Ofisi yake ilitangaza kuwa atasafiri kwenda Marekani kwa matibabu, na kuwa atarejea Namibia tarehe 2 Februari.
Geingob alichaguliwa kuwa Rais mnamo 2015 na amehudumu kwa mihula pili ambapo amefariki akiwa katika muhula wake wa pili.
Hage aliwahi kufanyiwa upasuaji, ambapo mwaka wa 2014 ilidaiwa kuwa amepona saratani ya kibofu.
Namibia inatazamiwa kufanya uchaguzi wa rais na wabunge mwezi Novemba 2024.
Chama tawala cha SWAPO, ambacho kimekuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1990, kimemchagua Nandi-Ndaitwah kama mgombea wake wa urais.
Kwa sasa pia ni Naibu Waziri Mkuu wa Namibia, na atakuwa Rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo iwapo atashinda.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria