Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Chongolo, amejiuzulu wadhifa huo, uamuzi ambao umeridhiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.
Kufuatia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia, ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwake, na ameridhia ombi hilo.
Hayo yamejiri jana jijini Dar es Salaam ambapo CCM ilifanya kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa chini ya Mwenyekiti wake Rais Samia.
Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilijadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hapa nchini.
Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimefanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoam, Mkoa wa Arusha: Wanachama waliojitokeza 89, walioteuliwa ni Dkt. Danie Pallangyo, Loy Sabaya, Solomon Kivuyo na Edin Kivuyo,
Kwa upanfe wa Mkoa wa Mbeya, wanachama waliojitokeza 48, Walioteuliwa ni Felix Iyaniva, Patrick Mwalunege na Fatuma Kasenga, Mkoa wa Mwanza, Wanachama waliojitokeza 109, walioteuliwa ni Michael Masanja, Sabana Salinja, Anjelina Samike, Elizabeth Nyingi na David Mulongo.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya Wilaya ya Mpanda: Wanachama waliojitokeza 36, walioteuliwa ni Hamis Sound, Joseph Lwamba, Josephina Baraga, na Emmanueli Manamba.
Wilaya ya Kusini Unguja wanachama waliojitokeza 15, walioteuliwa Maryam Haji, Ali Haji na Mohammed Haji Hassan
Aidha, kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.
More Stories
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha