December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Rais aendeleza uteuzi na uhamisho

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Bw. Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi Bw. Macha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  1. Amemteua Bi. Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi, Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  1. Amemteua Bw. Japahari Kubecha Mghamba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mghamba alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.
  1. Amemteua Bw. Mussa Kilakala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kilakala alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua.
  • Amemteua Bw. Robert Masunya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Masunya alikuwa Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Waanawake na Makundi Maalum.
  • Amemteua Bi. Mwashabani Mrope kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
  • Amemteua Bw. Jacob Simon Nkwera kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nkwera alikuwa Afisa Mwandamizi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
  • Amemteua Bw. Sangai Mambai kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Busega.
  1. Amemteua Bw. Raymond Mweli kuwa Katibu tawala wa Wilaya ya Kaliua.
  • Amemhamisha Bw. Frederick Damas Dagamiko kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga.
  • Amemhamisha Bw. Bashir Muhoja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
  • Amemhamisha Bw. Tito Philemon Mganwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Naibu Katibu Mkuu utafanyika tarehe 13 Machi, 2024 saa 04.00 asubuhi, Ikulu Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu