January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING NEWS: Rais aanza kuteua mawaziri, Kabudi na Mpango ndani

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Chamwino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Novemba, 2020 amefanya uteuzi wa Mawaziri 2 katika Baraza jipya la Mawaziri.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Pichani juu kushoto) kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Philip Isdor Mpango (pichani juu kulia) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Mawaziri Wateule hao walikuwa wakishikilia nyadhifa hizo katika Baraza la Mawaziri lililopita na uteuzi huu unaanza leo tarehe 13 Novemba, 2020.