NAIROBI, Mwandishi mashuri wa riwaya nchini Kenya, Profesa Ken Walibora amefariki dunia kwa kugongwa na daladala (matatu) katika barabara ya Ladhies jijini Nairobi.
Miongoni mwa riwaya zake maarufu za Kiswahili ni pamoja na Siku Njema ambayo ilichapishwa 1996.
Taarifa zilizolifikia Timesmajira Online zimethibitisha kuwa,Profesa huyo ambaye alikuwa hajaonekana tangu mwishoni mwa wiki aligongwa na matatu.
Mmoja wa marafiki wake wa karibu ambaye aliomba kutoandikwa jina lake aliueleza mtandao huu kuwa,mwili wa Profesa Walibora ulipelekwa katika Hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi kwa kutumia gari la dharura la Kaunti ya Nairobi.
Aidha, maafisa wa Jeshi la Polisi walielekea eneo la tukio ambapo walikuta simu yake ya mkononi ikiwa imeshikiliwa na watoto wanaoishi mazingira magumu na baadhi ya vielelezo.
“Alikuwa na kitambulisho na ufunguo wa gari, tayari familia yake imutambua mwili na wanasubiria mama yake aweze kufika,” alieleza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati Mark Wanjala.
Kwa habari hii na nyingine nyingi soma Gazeti la Majira.
More Stories
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza
Rais Samia atimiza ahadi Hanang
Daktari Dar ajishindia Mil. 100/- za Fainali NMB Bonge la Mpango