Na Doreen Aloyce, Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Momba, David Silinde (Chadema) ametangaza
kujiudhulu nafasi zake alizonazo ndani ya chama hicho kutokana na
kupata taarifa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa viongozi wa
CHADEMA wakimtaka ajiuzulu nyadhifa alizonazo.
Ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akizungumza na vyombo vya habari
kuhusiana na taarifa hizo. Alisema Mnadhimu Mkuu wa Upinzani, Esther
Bulaya amesambaza taarifa hizo kwenye mitandao.
Silinde amesema anashangazwa na taarifa za viongozi hao walizozitoa
kwenye mitandao zikimtaka ajiuzulu, kwani yeye binafsi alishauandikia
barua uongozi na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu,
John Mnyika kuwajulisha kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu wa wabunge na
msemaji wa kambi rasmi ya upinzani Wizara ya Viwanda na Biashara.
Habari kamili ipo katika gazeti huru la kila siku Majira…
More Stories
Mke wa Rais wa Msumbiji,Gueta atembelea JKCI
Kadinali Robert Prevost achaguliwa kuwa Papa Leo wa XIV
Viongozi wa Dini waaswa kuimarisha mafundisho kwa wanandoa kunusuru kuvunjika kwa ndoa